Huduma za Kifedha za Kuaminika

Mkopo nafuu, kwa haraka na uhakika.

Imarisha Maisha Financial Services hukuwezesha kupata mkopo ndani ya dakika 15 ukiwa ofisini. Mikopo ya magari, mikopo binafsi, bima na huduma za kifedha — zote sehemu moja.

Imeidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT)
Idhini ndani ya dakika 15
Matawi 5 nchini
Ofisi ya Imarisha Maisha Financial Services
Dakika 15Muda wa kupata mkopo
Matawi 5Dodoma, Dar, Mwanza, Mbeya

Tunafanya kazi na taasisi za kifedha zinazoaminika

CRDB Bank NMB Bank TPB Bank M-Pesa (Vodacom) Tigo Pesa Airtel Money
Huduma Zetu

Suluhisho la kifedha kwa kila hitaji

Kuanzia mikopo ya haraka hadi bima na huduma za malipo — tunakuhudumia kwa weledi na uwazi.

Mikopo Binafsi

Mikopo nafuu ya kukidhi mahitaji yako binafsi na ya kibiashara, kwa marejesho ya mwezi mmoja hadi miezi mitatu.

Jifunze zaidi

Mikopo ya Magari

Pata mkopo kwa dhamana ya gari, bajaji au pikipiki. Mchakato wa haraka na masharti rafiki.

Jifunze zaidi

Nunua Gari

Tunakusaidia kumiliki gari kupitia mpango wa malipo unaokubalika — chagua gari, lipa kidogo kidogo.

Jifunze zaidi

Huduma za Bima

Linda mali na maisha yako kupitia huduma zetu za bima zinazoaminika na za bei nafuu.

Wasiliana nasi

Huduma za Kifedha

M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, CRDB na NMB — tuma, pokea na lipa kwa urahisi sehemu moja.

Wasiliana nasi

Malipo ya Mkopo

Lipa mkopo wako kwa kutumia kumbukumbu namba (control number) kupitia CRDB, NMB au M-Pesa.

Hatua za malipo
Makao makuu ya Imarisha Maisha, Dodoma
Kwa Nini Sisi?

Tunaweka mteja mbele kwa kila hatua

Tumejijengea jina kwa kutoa huduma za haraka, nafuu na za uwazi. Mteja akifika ofisini, huhudumiwa ndani ya dakika 15 na kupokea kiasi alichoomba kwenye akaunti yake.

  • Mikopo yetu ni nafuu na yenye masharti rafiki
  • Huduma za haraka — idhini ndani ya dakika 15
  • Kwetu mteja ni Mfalme
  • Tuna uzoefu wa muda mrefu na uaminifu
15
Dakika kupata mkopo
5
Matawi nchini
4
Mikoa: Dodoma, Dar, Mwanza, Mbeya
100%
Mikopo hutolewa ofisini
Jinsi Inavyofanya Kazi

Pata mkopo kwa hatua nne rahisi

01

Tembelea Ofisi

Fika tawi letu lolote lililo karibu nawe ukiwa na vitambulisho husika.

02

Jaza Fomu

Jaza fomu ya maombi pamoja na dhamana (gari, bajaji au pikipiki).

03

Idhinishwa Haraka

Maombi yako huchakatwa na kuidhinishwa ndani ya dakika 15.

04

Pokea Fedha

Kiasi ulichoomba huingizwa moja kwa moja kwenye akaunti yako.

Wateja Wetu Wanasema

Wanaoamini huduma zetu

Binafsi huduma zenu ni nzuri, mnajali muda, mnawajali wateja na kuwasikiliza vizuri. Kwangu sijaona changamoto yoyote tangu nianze kuwa mteja wenu.

PD Paulina Jackson Dondo Mfanyabiashara

Huduma zenu ni nzuri, mnasaidia sana wakati mtu unapopatwa na dharura, hasa kwa wanaohitaji huduma ya fedha kwa haraka.

MB Mushobozi Davis Baitani Mfanyabiashara

Huduma zenu ni bora na zina mchango mkubwa katika maisha yangu. Nathamini jinsi mnavyohakikisha wateja wenu wanapata msaada unaohitajika.

DM Dennis Augustine Muchunguzi Mfanyabiashara

Ninachofurahishwa nacho zaidi kwenu ni namna mnavyowajali wateja wenu. Binafsi ningependa kusema huduma zenu ni nzuri na zinasaidia sana.

FN Faidha Athumani Ndalo Mfanyabiashara

Nashukuru kwa huduma bora mnazotoa. Ninavutiwa na jinsi mnavyowajali wateja wenu, na bila shaka huduma zenu ni za manufaa na zinatoa msaada mkubwa.

DM David Ernest Muwowo Mfanyabiashara

Nimefurahi sana na huduma mnazotoa. Inaonekana mnaweka juhudi nyingi kuhakikisha wateja wenu wanapata huduma za kipekee na zinazosaidia kwa hali yoyote.

AM Augustine Paschal Msizu Mfanyabiashara

Kiujumla niseme tu, huduma zenu ni nzuri sana. Na mmekuwa na utaratibu mzuri na wenye kuokoa muda katika kutoa huduma.

SK Seth Samwel Korosso Mfanyabiashara
Matawi Yetu

Tupo karibu nawe

Tembelea tawi letu lolote katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya.

Dodoma

Makao Makuu

Dar es Salaam

Dar es Salaam

Kijitonyama - Millennium Tower Na. 1 (+255) 675 362 511 (+255) 747 222 287

Mwanza

Mbeya

Tahadhari ya Usalama

Jilinde dhidi ya matapeli

Imarisha Maisha hatutoi mikopo kupitia mitandao ya simu wala hatutozi gharama yoyote ya awali. Mikopo yote hutolewa ofisini kwetu pekee. Akaunti zetu rasmi za mitandao ya kijamii ni @imarishamaishaltd tu (Instagram & Facebook).

Akaunti za matapeli za kuepuka:

imarisha_maisha imarisha_maisha_loans imarishamaisha imarisha_maisha_fasta kopa_mkopo_imarisha imarisha_maisha_mkopo_nafuu
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Una swali? Tuna majibu

Majibu ya maswali yanayoulizwa zaidi kuhusu mikopo na huduma zetu.

Unahitaji kitambulisho halali (NIDA, leseni ya udereva au pasipoti) na dhamana — gari, bajaji au pikipiki pamoja na nyaraka zake. Kisha fika tawi letu lolote lililo karibu nawe.
Mteja akikidhi vigezo na taratibu zote, mkopo hutolewa ndani ya dakika 15 ukiwa ofisini, na kiasi ulichoomba huingia kwenye akaunti yako ndani ya muda mfupi.
Mkopo wetu ni wa kuanzia mwezi mmoja, miwili hadi miezi mitatu. Marejesho hufanyika kila mwezi kulingana na mkopo uliouchagua.
Hapana. Hatutozi gharama zozote za awali kabla ya mteja kufika ofisini. Yeyote anayekuomba malipo ya awali ni tapeli — tafadhali epuka matapeli.
Hapana. Hatutoi mikopo kupitia M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money wala HaloPesa. Mikopo yote hutolewa ofisini kwetu pekee.
Unaweza kulipa kwa kutumia kumbukumbu namba (control number) kupitia CRDB, NMB au M-Pesa — kwa App, Wakala au benki. Angalia ukurasa wa Malipo kwa hatua kamili.
Tupo Dodoma (Makao Makuu), Dar es Salaam (Tabata-Segerea na Kijitonyama - Millennium Tower), Mwanza (Nyamanoro) na Mbeya (Uhindini).
Tayari Kuanza?

Boresha maisha yako leo na Imarisha Maisha

Omba mkopo mtandaoni au tembelea tawi letu lililo karibu nawe. Timu yetu iko tayari kukuhudumia.

Tuandikie WhatsApp